Karibu Mgeni, Fadhili Ingia | Register

Qatar imekuwa timu ya kwanza kubanduliwa nje ya Kombe la Dunia 2022

By - | Categories: Ulimwengu Tagi

Share this post:

 Khatari Qatar, wenyeji wa Kombe la Dunia 2022 wameondolewa katika hatua ya makundi. Walibanduliwa baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo katika Kundi A. Kwa maendeleo hayo, Qatar imekuwa nchi ya kwanza kutolewa kwenye mashindano hayo baada ya Uholanzi kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Ecuador. Matumaini ya Qatar kupata pointi tatu yalizimwa wakati Senegal ilipopepeta 3-1 katika mechi yao ya pili ya makundi. Wenyeji bado wanatakiwa kutimiza mechi yao iliyosalia dhidi ya kiongozi wa Kundi A Uholanzi jumanne katika uwanja wa Al Bayt. BBC iliripoti kuwa Qatar iliweka historia kwa kuwa nchi ya kwanza kutoka eneo la Mashariki ya Kati kuandaa Kombe la Dunia na sasa ina rekodi isiyohitajika ya kuwa timu ya pili tu ya nyumbani kuondoka kwenye mashindano hayo katika hatua ya makundi, baada ya Afrika Kusini mwaka 2010.